Kuhusu sisi

Utangulizi

Arusha One FM Radio ni kituo cha redio chenye makao makuu Jijini Arusha Tanzania. Arusha One inarusha matangazo yake kwenye masafa ya 101.7 Mhz, ikisika wilaya zote za mkoa wa Arusha na baadhi ya jirani kama vile Manyara, Kilimanjaro, Tanga na Dodoma.

Arusha One FM Radio imeanza kurusha matangazo yake mwaka 2007. Lengo kuu la radio hii ni kuelimisha na kuwaburudisha wasikilizaji wake. Lengo hili linatimizwa kwa kuandaa vipindi mbali mbali ili kukidhi mahitaji  yao ya kila siku.

Arusha One Radio inamilikiwa na Yahaya Abdallah (mkurugenzi mkuu), kwa kushirikiana na Iddy  Yahaya Njarita na Ibrahim Ally Mnzava. Arusha One FM ofisi kuu zinapatikana oljoro road ndani ya Green Valley School Block DD Plot No 436 Sombetini  Arusha.

Redio hii inawalenga sana wanafunzi,vijana na pia wananchi wa kawaida ambao ndio wengi nchini.Tunatangaza pia kupitia mitambo tofauti tofauti na hivyo basi tumejipatia idadi nyingi ya wasikilizaji tangu tulipoanza kurusha matangazo.

Maelezo Zaidi

Arusha One Redio FM  ni kituo cha kurusha matangazo kwa mawimbi ya sauti masaa 24 kupitia masafa ya 101.7 MHz kama ilivyoainishwa. Tumejikita zaidi katika kutafuta, kuandaa na kutangaza taarifa, maoni, hoja, kero na taarifa zinazogusa jamii katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo kama Elimu, Uchumi, Mazingira, Afya, Siasa, Dini, Uwajibikaji na harakati nyinginezo.

Kituo hiki cha kurusha matangazo kipo kata ya Sombetini barabara ya Oljoro Jijini Arusha kama inavyoonekana kwenye leseni ya biashara na usajili wa kibiashara Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania usajili namba 151375 na usajili wa mamlaka ya mawasiliano No TCRA/ CSRD/02/2015

Inashirikiana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na makampuni ya kifedha na yasiyo ya kifedha, ya umma na ya binafsi, viwanda , wafanyabiashara, watoa huduma muhimu kwa jamii na wengine wengi katika kuimarisha mahusiano mema, mawasiliano na ushirikiano mzuri wa jamii kutumia huduma au bidhaa toka kwa makampuni na wadau tajwa.

Hii ni kupitia matangazo ambayo hurushwa kwa gharama nafuu sana.

Faida kama utatangaza na Arusha One Redio FM, Bidhaa au huduma yako kujulikana, kupata wateja, kuwa mshinadani katika soko la kibiashara. Kuwa mdhani wa vipindi vyetu. Kualikwa kushiriki Mbashara katika kuelezea biashara, kupata furusa  yakutemelewa na watangazaji katika biashara yako, lakini kushiriki vikao na makongamano yahusuyo uhamasishaji wa matumizi ya bidhaa au huduma zako.

  Arusha One FM inaboresha maisha ya wasikilizaji wake kupitia taarifa za habari,za biashara, mazungumzo ya moja kwa moja, michezo, salamu na nyimbo tofauti tofauti kutoka ulimwengu mzima.

  Pia tunatengeneza matangazo mbalimbali,kutoa muda wa hewani kwa bei nafuu pamoja pamoja na kurusha matangazo ya bidhaa na huduma.Tunaandaa vipeperushi vya matangazo,kurekodi maigizo ya sauti, kurekodi na kutengrneza makala (Documentary).

  MAWASILIANO

  Block DD Plot No 436 Sombetini, Arusha

  SIMU

  0767118011/0677300406

  BARUA PEPE

  [email protected]